Thursday, April 28, 2016

IFAHAMU UWAWASE GROUP

IFAHAMU UWAWASE GROUP


Umoja wa wamiliki mashine za sembe, nawazalishaji wa sembe kwakifupi (UWAWASE GROUP)niumoja ulioanzishwa mnamo tarehe11/03/2014.

Mwanzo wa (UWAWASE GROUP) ni wajasiriamali wadogowadogo wenye viwanda yaani mashine za kuzalisha sembe/dona na wale wanaozalisha na kusambaza ndani ya Dar es salaam na nje ya Dar es salaam.

Wajasiriamali kwakuangalia mbali zaidi tumeona ni vyema tuwe na chombo chetukitakacho tuwezesha tuwe na kauli moja katika kujinasua na matatizo yanayo tukabili katika kuendesha shughuli zetu, bila kuingiliwa na taasisi nyingine ambayo haina dhamana na Umoja wetu.

Kwaujumla Umoja huu umehusisha wajasiriamali kutoka Manzese/Tandale na Dar es salaam kwa ujumla.

Umoja wetu umetokea kuwavutia wanaumoja wengi ambao wanashughulika na usindikaji wa mahindi ya sembe na dona maeneo yote ya Dar es salaam.

Umoja wetu una katiba ambayo kila mwanaumoja anatakiwa kuiheshimu, kuifuata na kuisimamia maana ndio muongozo wa Umoja wetu.

Katiba ya umoja wetu imetungwa nakupitishwa na wajumbe wote wa UWAWASE GROUP.

Extract from Register
Business Name No280324 Date of Registration 11-Mar-14
Name of Business: UWAWASE GROUP

Certificate of Registration
The Business Names(Registration) Act (Cap 213)

I hereby certify that UWAWASE GROUP
Share:

0 comments:

Post a Comment