Monday, May 2, 2016
MALENGO YA UMOJA WA UWAWASE GROUP
MALENGO YA
UMOJA WA UWAWASE GROUP
11. Kuwaunganisha wamiliki na mashine na
wazalishaji Sembe/Dona katika mkoa wa Dar es Salaam na vuinga vyake.
2. Kuhakikisha tunazalisha Sembe bora
ili kulinda afya za walaji.
3. Kutafuta na kufuatilia soko la malighafi
(mahindi) popote ndani na nje ya Tanzania ili kukidhi haja na mahitaji ya
wanaUwawase Group.
4. Kutafuta na Kufuatilia Soko la
Sembe/Dona popote ndani na nje ya Tanzania kwa ajili ya wanaUwawase Group kuuza
Sembe/Dona zao.
5. Kuwa na soko la bei moja wakati wa
kununua mahindi na kuuza Sembe/Dona.
6. Kutetea na kulinda maslahi ya
wanachama.
7. Kukusanya kiingilio, Ada na mapato
mengine yatakayowaletea maendeleo ya wanaumoja.
8. Kubuni, kuzianzisha na kuendeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuongeza mapato ya Chama na kuboresha maisha
ya wanachama.
9. Kuitangaza na kuiunganisha Uwawase na
taasisi za serikali na zisizo za serikali ili kupata huduma stahiki kwa Chama
na wanachama.
10.
Kufanya
Uwawase kuwa katika kundi la wawekezaji wa ndani wa viwanda vidogo vya kati
katika uzalishaji wa usambazaji wa Sembe/dona bora ndani na nje ya Tanzania.
11.
Kutafuta
njia rahisi ya kupata mitaji ya kustawisha viwanda na biashara ya wanauwawase
group.
12.
Kuwa
taasisi/Umoja mkubwa unaojitosheleza katika tasinia hii ya uwezeshaji wa
viwanda vya kuongeza dhamani ya mahindi.
WAJIBU WA MWANAUMOJA WA UWAWASE GROUP
WAJIBU WA MWANAUMOJA
WA UWAWASE GROUP
Mwanaumoja
atawajibika kutimiza wajibu wakekulingana na katiba na makubaliano yaliofikiwa
na umoja wetu kwa ujumla, kupitia mkutano mkuu wetu kufanya yafuatayo:-
1.
Kuhudhuria mikutano yote ya umoja wetu.
2. Kulipa
ada kila mwanzo wa mwezi kwa wakati.
3. Kulipa
michango yote ile ya dharura na ile ya lazima kama msiba.
4. Kulinda
mali zote za umoja.
5. Kufanya
kazi za umoja kwa kujitolea.
6. Kushiriki
kwenye shughuli zote za wanaumoja.
7.
Kutokusambaza taarifa zisizo kuwa zakweli zihusuzo
umoja wetu.
8. Kushauri
au wetu, kutoa maoni juu ya ustawi wa umoja.
UTARATIBU WA VIKAO VYA UMOJA WA UWAWASE GROUP
UTARATIBU WA VIKAO VYA UMOJA WA UWAWASE GROUP
1.
Mwana Umoja ambae atashindwa
kuhudhuria mikutano mara nne atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye umoja na kama
kuna haki yoyote kwenye umoja atakuwa ameipoteza.
2. Mwana umoja atahudhuria mkutano kila baada ya miezi mitatu.
3. Wajumbe wa kamati ya utendaji watakutana kila inapo bidi kufanya
hivyo.
4. Mkutano mkuu wa umoja utafanyika mara moja kwa mwaka.
UONGOZI NA KAMATI ZA UONGOZI WA UWAWASE GROUP
UONGOZI NA KAMATI ZA UONGOZI WA UWAWASE GROUP
USIMAMIZI/UWONGOZI.
1. Madaraka
makuu yanayo husu UWAWASE GROUP yatakuwa kwa wana umoja wenyewe kwenye mikutano
mikuu.
2. Kutakuwa
na mikutano mikuu ya UWAWASE GROUP (3)
i)
Mkutano mkuu ya mwaka.
ii) Mkutano
kila baada ya miezi mitatu.
iii) Mkutano
wa dharura.
3.2
Kufanya uchaguzi wa viongozi wa UWAWASE
GROUP.
3.3
Kujadili na kutoa mapendekezo ya miradi
ya UWAWASE GROUP.
3.4
Kuidhinisha mauzo au manunuzi ya mali za
UWAWASE GROUP.
3.5
Kutaundwa kamati ndogondogo za uwongozina
zitakuwa na mamlaka ya kutambuliwa na wana UWAWASE GROUP.
VIONGOZI.
UWAWASE
GROUP, Itaongozwa na viongozi wafuatao:-
1. Mwenyekiti
2. Makamu
mwenyekiti
3. Katibu
4. Katibu
msaidizi
5. Mtunza
Hazina
Viongozi
hawa watapigiwa kura ya siri na wajumbe wa mkutano mkuu wa umoja .
6.1
Muda wa uongozi wa UWAWASE GROUP ni miaka mitatu tu.
6.2
Idadi ya wapiga kura kwenye mkutano mkuu italazimika wajumbe wafike zaidi ya nusu
ya
wanaumoja wote.
1.3 Wajumbe
wa mkutano mkuu watateua kamati itakayosimamia mambo ya katiba, sheria
nanidhamu ya umoja.
6.4
Kamati ya utendaji itakuwa na wajibu wa kuunda kamati mbalimbali zitakazo
imarisha
utendaji
wa umoja.
6.5
Kiongozi anaweza kuongoza mihula miwili kama ataonekena anafaa kufanya hivyo na
wanaumoja.
WAJIBU
WA VIONGOZI.
MWENYEKITI.
a. Mwenyekiti;
ataendesha vikao vyote vya umoja ndie msemaji mkuu katika mikutano yote na
kutoa miongozo kwa kila jambo ndani na nje ya mkutano wa umoja.
b. Mwenyekiti;
msaidizi huyu atafanya shughuli zote za mwenyekiti kwa kutumwa na mwenyekiti au
pindi mwenyekiti anapokuwa hayupo.
KATIBU.
a. Katibu,
atakuwa ndiemtendaji mkuu wa umoja kwa shughuli zote zakiutendajikwa wana umoja
pia ataandika taarifa zote za mikutano na kutunza kumbukumbu zote za vikao
halali vya umoja,na atakuwa na mawasiliano ya marakwamara kati ya uongozi na wanaumoja kuhusu taarifa zozote zinazo wahusu
wanaumoja.
b. Katibu
msaidizi atafanya shughuli zote za katibukwa kushirikiana na pindi katibu mkuu
atakapokuwa hayup atakaimu.
MTUNZA
HAZINA.
a. Atahakikisha
anafuata taratibu zote za uhifadhiwa fedha za umoja.
b. Atapokea
pesa na kutoa risiti kwa mwanaumoja yeyote atakae toa pesa zihusuzo umoja.
c. Atafanya
malipo pale atakapo takiwa kufanya hivyo na kamati ya fedha ya umoja kwa
kushirikiana na watia saini baada ya kulipishwa na kamati ya utendaji.
d. Atahakikisha
hesabu zote za fedha ya umoja ndiye atazitolea maelezo ya mapato na matumizi
pale atakapotakiwa kufanya hivyo na kikao halali cha umoja.
e. Atatunza
vitabu vyote vya risiti na hesabu za umoja.
f. Atakusanya
na kupeleka pesa bank kila mara.
g. Ataandaa
hesabu zote za umoja na kuziwakilisha kwenye kikao/mkutano husika.
h. Atashauri
kamati ya fedha juu ya matumizi ya umoja yenye tija.
i.
Atashirikiana na kamati ya fedha kuandaa
bajeti ya matumizi ya umoja pale inapotakiwa kufanya hivyo.
KAMATI
YA UTENDAJI.
Kamati
hii ndiyo kamati ambayo inatakiwa kuwa makini kwa kuhakikisha inafanya mambo ya
kiutendajizaidi.
1. Itapokea
na kutekeleza maelekezo yote kutoka mkutano mkuu wa umoja
2. Itafuatilia
kazi na maelekezo mbalimbali yanayo husu umoja wetu
3. Itahusika
kutoa maelekezo ya kiutendaji kwa kamati mbalimbali za umoja wetu.
4. Itaitisha
mkutano wa dharura kujadili jambo lolote jipya kwa wanaumoja.
5. Itakuwa
na jukumu la kumuhidhinisha mwanaumoja mpya baada ya kupokea barua yake ya
maombi ya kujiunga na umoja iliyokuwisha jadiliwa na kamati ya katiba na sheria.
6. Itabuni
na kuanzisha mradi au jambo lolote maslahi kwa wanaumoja baada ya kukubaliwa na
mkutano mkuu.
7. Itazingatia
maslai ya umoja zaidi kuliko vinginevyo.
KAMATI
YA KATIBA SHERIA NA NIDHAMU.
Kamati
hii itakuwa ndiyo msingi wa umoja wetu kwa kuhakikisha inafanya mambo yake kwa
werevu mkubwa huku ikijuwa kuwa ndio
tegemeo kubwa la kisheria la umoja, nayo itateuliwa kupitia mkutano mkuu wa
wanaumoja, hatahivyo itakuwa kamati huru, kamati hii itasimamia uchaguzi wa
viongozi kipindi cha uchaguzi, pia
itafanya yafuatayo:-
a. Kusimamia
utekelezwaji wa maelekezo ya katiba ya umoja.
b. Kusimamia
maboresho ya katiba ya umoja pindi itakapo lazimika kufanya hivyo.
c. Kuhakikisha
kila kiongozi/mwanaumoja anatii na kufuata sheria hizo
d. Kudhibiti
mwiingiliano wa uongozi katika umoja.
e. Kuunda
sheria ndogondogo zitakazo ongoza umoja wetu.
f. Kuhakikisha
viongozi wa umoja wanatii na kuilinda katiba katika utendaji wao
g. Kusimamia
adhabu kwa mwana umoja kutokana na kosa alilofanya.
h. Kushauriana
na kamati ya utendaji juu ya kufanya mikataba mbalimbali inayohusu umoja wetu.
i.
Kupokea na kujadili barua ya barua ya
maombi mapya kabla ya kuidhinishwa na kamati ya utendaji.
j.
Kamati hii pamoja na kuwa huru itafanya
kazi kwa karibu na chini ya kamati ya utendaji kwa maslahi ya wanauwawase
group.
UENDESHAJI WA MASUALA YA KIFEDHA NDANI YA UWAWASE GROUP
UENDESHAJI WA MASUALA YA KIFEDHA NDANI YA UWAWASE GROUP
VYANZO VYA MAPATO.
1. Kiingilio.
2. Ada.
3. Mikopo
ya bank/Taasisi za fedha.
4. Msaada
toka kwa wafadhili
5. Mauzo
ya nakala ya katiba.
6. Mauzo
ya vitabu vya sheria ndogondogo za umoja.
7. Michango
mbalimbali kutoka kwa taasisi zisizokuwa za serikali za ndani na nje ya nchi,
vitu halisi au fedha.
4.1
MATUMIZI YA MAPATO.
Umoja
huu uta hakikisha una yatumia ipasavyo mapato yote yaliyopatikana kwa njia tajwa
hapo juu yaani (4.0 1hadi 7)kwa kufanya mambo yafuatayo:-
1. Kulipa
pango la ofisi ya Uwawase Group.
2. Kumpa
rambirambi mfiwa au marehemu kwataratibu tuliojiwekea.
3. Kusaidia
jitihada za kutafuta malighafi (mahindi) popote pale ili kuwafanya wanaumoja
kupata mahindi hasa kipindi cha upungufu wa mahindi.
4. Ikibidi
hata kufanya mawasiliano na nje ya nchi kufanikisha kupata mahindi.
5. Kuendesha
shughuli zote za ofisi ya UWAWASE GROUP, pamoja na kugharamia matumizi ya
ofisi.
6. Kulipa
watumishi wa ofisi kama Karani/Secretary, mlinzi, na viongozi kwa shughuli
maalum za ofisi na ufuatiliaji nje ya ofisi kwa manuafaa ya umoja wetu.
7. Ikifikia
wakati tuibue vitega uchumi mbalimbali kuimarisha mfuko wetu.
8. Kugharamia
mikutano yote ya Uwawase Group.
9. Kutimiza
malengo ya umoja yaliyopitishwa na mkutano mkuu.
4.2
VITU HALISIYA.
a) Iwapo
mtu au taasisi itafanya shughuli na UWAWASE GROUP na ikafanikiwa kujitolea
vifaa au pesa, kwaajili ya utekelezaji wa mpango wowote UWAWASE GROUP haitalipa
wala kugharamia uharibifu wowote utakaojitokeza.
b) UWAWASE
GROUP itabaki kuwa ndio mmiliki mkuu wa mali na wanaumoja wake,bila kuingiliana
na taasisi yoyote ile iliyoshirikishwa.
4.3
ASASI ZA FEDHA.
a) Iwapo
mkutano mkuu ukiona kuna umuhimu wa kupatapesa kutoka benki kwa haraka katika
umoja wetu kwaajili ya kufanya jambo kwa maramoja na lenye malengo mema
kimaendeleo, basi mkutano mkuu utatoa idhini kwa kamati ya utendaji kufanya
hivyo chini ya taratibu ambazo mkutano mkuu utakuwa umeziweka/kuridhia kwa
pamoja.
b) Wanaumoja
watakaopitisha azimio hili la kukopa pesa au bank katika Taasisi kipesa
zilizoruhusiwa kisheria lazima liwe theluthi tatu ya wanaumoja wote.
4.4
UHIFADHI WA FEDHA.
1. Umoja
utahifadhi pesa zake bank.
2. Sehemu
ya pesa ndogondogo zinazohitajika kwa matumizi ya kiofisi yatahifadhiwa kwa
taratibu zitakazowekwa na uongozi kwa mtunza fedha,
3. Tunaweza
kuwekeza fedha kwa kununuwa hisa au mali isiyo hamishika kama nyumba, kiwanja/shamba
kwa makubaliano ya wanaumoja kupitia mkutano mkuu.
4. Mwaka
wa fedha wa umoja utaanza Januari na kuishia DIsemba.
5. Umoja
utaandaa hesabu zake na kuzitunza kwa utaratibu ulioandaliwa na wanaumoja
wenyewe.
6. Kamati
ya mipango, uchumi nafedha ya umoja itapitia taarifa ya fedha kila baada ya
miezi mitatu na kuiwasilisha kwenye mkutano wa wanaumoja.
7. Wajumbe
wa kamati yamipango, uchumi na fedha watakuwa na idhini ya kupitia manunuzi,
matumizi, na mapato yote yaliyofanyika kwenye umoja.
8. Ukaguzi,kuundwe
kamati ya dharura ya ukaguzi wa hesabu za mwaka kutoka kwa wana umoja wenyewekamati
hiyo isizidi watu watano kwa ukaguzi wa hesabu za ndani(mtaalam wa
hesabu/mahesabu).
9. Muda
wa kamati ya ukaguzi utakoma baada ya kumaliza hesabu hizo ndani ya mwezi
mmoja.
10. Gharama
za kamati ya ukaguzi zitalipwa na mfuko wa umoja wenyewe.











