Monday, May 2, 2016

UENDESHAJI WA MASUALA YA KIFEDHA NDANI YA UWAWASE GROUP


UENDESHAJI WA MASUALA YA KIFEDHA NDANI YA UWAWASE GROUP





    VYANZO VYA MAPATO.
1.      Kiingilio.
2.      Ada.
3.      Mikopo ya bank/Taasisi za fedha.
4.      Msaada toka kwa wafadhili
5.      Mauzo ya nakala ya katiba.
6.      Mauzo ya vitabu vya sheria ndogondogo za umoja.
7.      Michango mbalimbali kutoka kwa taasisi zisizokuwa za serikali za ndani na nje ya nchi, vitu halisi au fedha.

4.1 MATUMIZI YA MAPATO.
Umoja huu uta hakikisha una yatumia ipasavyo mapato yote yaliyopatikana kwa njia tajwa hapo juu yaani (4.0 1hadi 7)kwa kufanya mambo yafuatayo:-
1.      Kulipa pango la ofisi ya Uwawase Group.
2.      Kumpa rambirambi mfiwa au marehemu kwataratibu tuliojiwekea.
3.      Kusaidia jitihada za kutafuta malighafi (mahindi) popote pale ili kuwafanya wanaumoja kupata mahindi hasa kipindi cha upungufu wa mahindi.
4.      Ikibidi hata kufanya mawasiliano na nje ya nchi kufanikisha kupata mahindi.
5.      Kuendesha shughuli zote za ofisi ya UWAWASE GROUP, pamoja na kugharamia matumizi ya ofisi.
6.      Kulipa watumishi wa ofisi kama Karani/Secretary, mlinzi, na viongozi kwa shughuli maalum za ofisi na ufuatiliaji nje ya ofisi kwa manuafaa ya umoja wetu.
7.      Ikifikia wakati tuibue vitega uchumi mbalimbali kuimarisha mfuko wetu.
8.      Kugharamia mikutano yote ya Uwawase Group.
9.      Kutimiza malengo ya umoja yaliyopitishwa na mkutano mkuu.



4.2 VITU HALISIYA.
a)      Iwapo mtu au taasisi itafanya shughuli na UWAWASE GROUP na ikafanikiwa kujitolea vifaa au pesa, kwaajili ya utekelezaji wa mpango wowote UWAWASE GROUP haitalipa wala kugharamia uharibifu wowote utakaojitokeza.

b)      UWAWASE GROUP itabaki kuwa ndio mmiliki mkuu wa mali na wanaumoja wake,bila kuingiliana na taasisi yoyote ile iliyoshirikishwa.

4.3 ASASI ZA FEDHA.
a)      Iwapo mkutano mkuu ukiona kuna umuhimu wa kupatapesa kutoka benki kwa haraka katika umoja wetu kwaajili ya kufanya jambo kwa maramoja na lenye malengo mema kimaendeleo, basi mkutano mkuu utatoa idhini kwa kamati ya utendaji kufanya hivyo chini ya taratibu ambazo mkutano mkuu utakuwa umeziweka/kuridhia kwa pamoja.

b)      Wanaumoja watakaopitisha azimio hili la kukopa pesa au bank katika Taasisi kipesa zilizoruhusiwa kisheria lazima liwe theluthi tatu ya wanaumoja wote.



4.4 UHIFADHI WA FEDHA.
1.      Umoja utahifadhi pesa zake bank.
2.      Sehemu ya pesa ndogondogo zinazohitajika kwa matumizi ya kiofisi yatahifadhiwa kwa taratibu zitakazowekwa na uongozi kwa mtunza fedha,
3.      Tunaweza kuwekeza fedha kwa kununuwa hisa au mali isiyo hamishika kama nyumba, kiwanja/shamba kwa makubaliano ya wanaumoja kupitia mkutano mkuu.
4.      Mwaka wa fedha wa umoja utaanza Januari na kuishia DIsemba.
5.      Umoja utaandaa hesabu zake na kuzitunza kwa utaratibu ulioandaliwa na wanaumoja wenyewe.
6.      Kamati ya mipango, uchumi nafedha ya umoja itapitia taarifa ya fedha kila baada ya miezi mitatu na kuiwasilisha kwenye mkutano wa wanaumoja.
7.      Wajumbe wa kamati yamipango, uchumi na fedha watakuwa na idhini ya kupitia manunuzi, matumizi, na mapato yote yaliyofanyika kwenye umoja.
8.      Ukaguzi,kuundwe kamati ya dharura ya ukaguzi wa hesabu za mwaka kutoka kwa wana umoja wenyewekamati hiyo isizidi watu watano kwa ukaguzi wa hesabu za ndani(mtaalam wa hesabu/mahesabu).
9.      Muda wa kamati ya ukaguzi utakoma baada ya kumaliza hesabu hizo ndani ya mwezi mmoja.

10.  Gharama za kamati ya ukaguzi zitalipwa na mfuko wa umoja wenyewe.
Share:

0 comments:

Post a Comment