MALENGO YA
UMOJA WA UWAWASE GROUP
11. Kuwaunganisha wamiliki na mashine na
wazalishaji Sembe/Dona katika mkoa wa Dar es Salaam na vuinga vyake.
2. Kuhakikisha tunazalisha Sembe bora
ili kulinda afya za walaji.
3. Kutafuta na kufuatilia soko la malighafi
(mahindi) popote ndani na nje ya Tanzania ili kukidhi haja na mahitaji ya
wanaUwawase Group.
4. Kutafuta na Kufuatilia Soko la
Sembe/Dona popote ndani na nje ya Tanzania kwa ajili ya wanaUwawase Group kuuza
Sembe/Dona zao.
5. Kuwa na soko la bei moja wakati wa
kununua mahindi na kuuza Sembe/Dona.
6. Kutetea na kulinda maslahi ya
wanachama.
7. Kukusanya kiingilio, Ada na mapato
mengine yatakayowaletea maendeleo ya wanaumoja.
8. Kubuni, kuzianzisha na kuendeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuongeza mapato ya Chama na kuboresha maisha
ya wanachama.
9. Kuitangaza na kuiunganisha Uwawase na
taasisi za serikali na zisizo za serikali ili kupata huduma stahiki kwa Chama
na wanachama.
10.
Kufanya
Uwawase kuwa katika kundi la wawekezaji wa ndani wa viwanda vidogo vya kati
katika uzalishaji wa usambazaji wa Sembe/dona bora ndani na nje ya Tanzania.
11.
Kutafuta
njia rahisi ya kupata mitaji ya kustawisha viwanda na biashara ya wanauwawase
group.
12.
Kuwa
taasisi/Umoja mkubwa unaojitosheleza katika tasinia hii ya uwezeshaji wa
viwanda vya kuongeza dhamani ya mahindi.







0 comments:
Post a Comment