Monday, May 2, 2016

UONGOZI NA KAMATI ZA UONGOZI WA UWAWASE GROUP

UONGOZI NA KAMATI ZA UONGOZI WA UWAWASE GROUP






USIMAMIZI/UWONGOZI.
1.      Madaraka makuu yanayo husu UWAWASE GROUP yatakuwa kwa wana umoja wenyewe kwenye mikutano mikuu.
2.      Kutakuwa na mikutano mikuu ya UWAWASE GROUP (3)
i)        Mkutano mkuu ya mwaka.
ii)      Mkutano kila baada ya miezi mitatu.
iii)    Mkutano wa dharura.
3.2              Kufanya uchaguzi wa viongozi wa UWAWASE GROUP.
3.3              Kujadili na kutoa mapendekezo ya miradi ya UWAWASE GROUP.
3.4              Kuidhinisha mauzo au manunuzi ya mali za UWAWASE GROUP.
3.5              Kutaundwa kamati ndogondogo za uwongozina zitakuwa na mamlaka ya kutambuliwa na wana UWAWASE GROUP.



 VIONGOZI.
UWAWASE GROUP, Itaongozwa na viongozi wafuatao:-
1.      Mwenyekiti
2.      Makamu mwenyekiti
3.      Katibu
4.      Katibu msaidizi
5.      Mtunza Hazina
Viongozi hawa watapigiwa kura ya siri na wajumbe wa mkutano mkuu wa umoja .
6.1 Muda wa uongozi wa UWAWASE GROUP ni miaka mitatu tu.
6.2 Idadi ya wapiga kura kwenye mkutano mkuu italazimika wajumbe wafike zaidi ya nusu
ya wanaumoja wote.
1.3  Wajumbe wa mkutano mkuu watateua kamati itakayosimamia mambo ya katiba, sheria nanidhamu ya umoja.
6.4 Kamati ya utendaji itakuwa na wajibu wa kuunda kamati mbalimbali zitakazo imarisha
utendaji wa umoja.
6.5 Kiongozi anaweza kuongoza mihula miwili kama ataonekena anafaa kufanya hivyo na
wanaumoja.

WAJIBU WA VIONGOZI.

MWENYEKITI.
a.       Mwenyekiti; ataendesha vikao vyote vya umoja ndie msemaji mkuu katika mikutano yote na kutoa miongozo kwa kila jambo ndani na nje ya mkutano wa umoja.
b.      Mwenyekiti; msaidizi huyu atafanya shughuli zote za mwenyekiti kwa kutumwa na mwenyekiti au pindi mwenyekiti anapokuwa hayupo.



KATIBU.
a.       Katibu, atakuwa ndiemtendaji mkuu wa umoja kwa shughuli zote zakiutendajikwa wana umoja pia ataandika taarifa zote za mikutano na kutunza kumbukumbu zote za vikao halali vya umoja,na atakuwa na mawasiliano ya marakwamara kati ya uongozi na  wanaumoja kuhusu taarifa zozote zinazo wahusu wanaumoja.

b.      Katibu msaidizi atafanya shughuli zote za katibukwa kushirikiana na pindi katibu mkuu atakapokuwa hayup atakaimu.

MTUNZA HAZINA.
a.       Atahakikisha anafuata taratibu zote za uhifadhiwa fedha za umoja.
b.      Atapokea pesa na kutoa risiti kwa mwanaumoja yeyote atakae toa pesa zihusuzo umoja.
c.       Atafanya malipo pale atakapo takiwa kufanya hivyo na kamati ya fedha ya umoja kwa kushirikiana na watia saini baada ya kulipishwa na kamati ya utendaji.
d.      Atahakikisha hesabu zote za fedha ya umoja ndiye atazitolea maelezo ya mapato na matumizi pale atakapotakiwa kufanya hivyo na kikao halali cha umoja.
e.       Atatunza vitabu vyote vya risiti na hesabu za umoja.
f.       Atakusanya na kupeleka pesa bank  kila mara.
g.      Ataandaa hesabu zote za umoja na kuziwakilisha kwenye kikao/mkutano husika.
h.      Atashauri kamati ya fedha juu ya matumizi ya umoja yenye tija.
i.        Atashirikiana na kamati ya fedha kuandaa bajeti ya matumizi ya umoja pale inapotakiwa kufanya hivyo.
j.        Atafanya kazi kwa kufuata taratibu za umoja chini ya mwenyekiti na katibu wa Uwawase Group.



KAMATI YA UTENDAJI.
Kamati hii ndiyo kamati ambayo inatakiwa kuwa makini kwa kuhakikisha inafanya mambo ya kiutendajizaidi.
1.      Itapokea na kutekeleza maelekezo yote kutoka mkutano mkuu wa umoja
2.      Itafuatilia kazi na maelekezo mbalimbali yanayo husu umoja wetu
3.      Itahusika kutoa maelekezo ya kiutendaji kwa kamati mbalimbali za umoja wetu.
4.      Itaitisha mkutano wa dharura kujadili jambo lolote jipya kwa wanaumoja.
5.      Itakuwa na jukumu la kumuhidhinisha mwanaumoja mpya baada ya kupokea barua yake ya maombi ya kujiunga na umoja iliyokuwisha  jadiliwa na kamati ya katiba  na sheria.
6.      Itabuni na kuanzisha mradi au jambo lolote maslahi kwa wanaumoja baada ya kukubaliwa na mkutano mkuu.
7.      Itazingatia maslai ya umoja zaidi kuliko vinginevyo.


KAMATI YA KATIBA SHERIA NA NIDHAMU.
Kamati hii itakuwa ndiyo msingi wa umoja wetu kwa kuhakikisha inafanya mambo yake kwa werevu  mkubwa huku ikijuwa kuwa ndio tegemeo kubwa la kisheria la umoja, nayo itateuliwa kupitia mkutano mkuu wa wanaumoja, hatahivyo itakuwa kamati huru, kamati hii itasimamia uchaguzi wa viongozi  kipindi cha uchaguzi, pia itafanya yafuatayo:-
a.       Kusimamia utekelezwaji wa maelekezo ya katiba ya umoja.
b.      Kusimamia maboresho ya katiba ya umoja pindi itakapo lazimika kufanya hivyo.
c.       Kuhakikisha kila kiongozi/mwanaumoja anatii na kufuata sheria hizo
d.      Kudhibiti mwiingiliano wa uongozi katika umoja.
e.       Kuunda sheria ndogondogo zitakazo ongoza umoja wetu.
f.       Kuhakikisha viongozi wa umoja wanatii na kuilinda katiba katika utendaji wao
g.      Kusimamia adhabu kwa mwana umoja kutokana na kosa alilofanya.
h.      Kushauriana na kamati ya utendaji juu ya kufanya mikataba mbalimbali inayohusu umoja wetu.
i.        Kupokea na kujadili barua ya barua ya maombi mapya kabla ya kuidhinishwa na kamati ya utendaji.

j.        Kamati hii pamoja na kuwa huru itafanya kazi kwa karibu na chini ya kamati ya utendaji kwa maslahi ya wanauwawase group.


Share:

0 comments:

Post a Comment