Monday, May 2, 2016

UWAWASE GROUP KATIKA SEMINA ELEKEZI NA UHIFADHI BORA WA CHAKULA NA VIRUTUBISHO (PICHA)

UWAWASE GROUP KATIKA SEMINA ELEKEZI YA UHIFADHI BORA WA CHAKULA NA VIRUTUBISHO (PICHA)











Share:

MALENGO YA UMOJA WA UWAWASE GROUP

MALENGO YA UMOJA WA UWAWASE GROUP

11.    Kuwaunganisha wamiliki na mashine na wazalishaji Sembe/Dona katika mkoa wa Dar es Salaam na vuinga vyake.

2.    Kuhakikisha tunazalisha Sembe bora ili kulinda afya za walaji.

3.    Kutafuta na kufuatilia soko la malighafi (mahindi) popote ndani na nje ya Tanzania ili kukidhi haja na mahitaji ya wanaUwawase Group.

4.    Kutafuta na Kufuatilia Soko la Sembe/Dona popote ndani na nje ya Tanzania kwa ajili ya wanaUwawase Group kuuza Sembe/Dona zao.

5.    Kuwa na soko la bei moja wakati wa kununua mahindi na kuuza Sembe/Dona.

6.    Kutetea na kulinda maslahi ya wanachama.

7.    Kukusanya kiingilio, Ada na mapato mengine yatakayowaletea maendeleo ya wanaumoja.

8.    Kubuni, kuzianzisha na kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuongeza mapato ya Chama na kuboresha maisha ya wanachama.

9.    Kuitangaza na kuiunganisha Uwawase na taasisi za serikali na zisizo za serikali ili kupata huduma stahiki kwa Chama na wanachama.

10.                       Kufanya Uwawase kuwa katika kundi la wawekezaji wa ndani wa viwanda vidogo vya kati katika uzalishaji wa usambazaji wa Sembe/dona bora ndani na nje ya Tanzania.

11.                       Kutafuta njia rahisi ya kupata mitaji ya kustawisha viwanda na biashara ya wanauwawase group.

12.                       Kuwa taasisi/Umoja mkubwa unaojitosheleza katika tasinia hii ya uwezeshaji wa viwanda vya kuongeza dhamani ya mahindi.
Share:

WAJIBU WA MWANAUMOJA WA UWAWASE GROUP

WAJIBU WA MWANAUMOJA WA UWAWASE GROUP


Mwanaumoja atawajibika kutimiza wajibu wakekulingana na katiba na makubaliano yaliofikiwa na umoja wetu kwa ujumla, kupitia mkutano mkuu wetu kufanya yafuatayo:-
1.    Kuhudhuria mikutano yote ya umoja wetu.
2.  Kulipa ada kila mwanzo wa mwezi kwa wakati.
3.  Kulipa michango yote ile ya dharura na ile ya lazima kama msiba.
4.  Kulinda mali zote za umoja.
5.  Kufanya kazi za umoja kwa kujitolea.
6.  Kushiriki kwenye shughuli zote za wanaumoja.
7.   Kutokusambaza taarifa zisizo kuwa zakweli zihusuzo umoja wetu.

8.  Kushauri au wetu, kutoa maoni juu ya ustawi wa umoja.
Share:

UTARATIBU WA VIKAO VYA UMOJA WA UWAWASE GROUP

UTARATIBU WA VIKAO VYA UMOJA  WA UWAWASE GROUP


1.    Mwana Umoja ambae atashindwa kuhudhuria mikutano mara nne atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye umoja na kama kuna haki yoyote kwenye umoja atakuwa ameipoteza.

2.  Mwana umoja atahudhuria mkutano kila baada ya miezi mitatu.

3.  Wajumbe wa kamati ya utendaji watakutana kila inapo bidi kufanya hivyo.

4.  Mkutano mkuu wa umoja utafanyika mara moja kwa mwaka.


Share:

UONGOZI NA KAMATI ZA UONGOZI WA UWAWASE GROUP

UONGOZI NA KAMATI ZA UONGOZI WA UWAWASE GROUP






USIMAMIZI/UWONGOZI.
1.      Madaraka makuu yanayo husu UWAWASE GROUP yatakuwa kwa wana umoja wenyewe kwenye mikutano mikuu.
2.      Kutakuwa na mikutano mikuu ya UWAWASE GROUP (3)
i)        Mkutano mkuu ya mwaka.
ii)      Mkutano kila baada ya miezi mitatu.
iii)    Mkutano wa dharura.
3.2              Kufanya uchaguzi wa viongozi wa UWAWASE GROUP.
3.3              Kujadili na kutoa mapendekezo ya miradi ya UWAWASE GROUP.
3.4              Kuidhinisha mauzo au manunuzi ya mali za UWAWASE GROUP.
3.5              Kutaundwa kamati ndogondogo za uwongozina zitakuwa na mamlaka ya kutambuliwa na wana UWAWASE GROUP.



 VIONGOZI.
UWAWASE GROUP, Itaongozwa na viongozi wafuatao:-
1.      Mwenyekiti
2.      Makamu mwenyekiti
3.      Katibu
4.      Katibu msaidizi
5.      Mtunza Hazina
Viongozi hawa watapigiwa kura ya siri na wajumbe wa mkutano mkuu wa umoja .
6.1 Muda wa uongozi wa UWAWASE GROUP ni miaka mitatu tu.
6.2 Idadi ya wapiga kura kwenye mkutano mkuu italazimika wajumbe wafike zaidi ya nusu
ya wanaumoja wote.
1.3  Wajumbe wa mkutano mkuu watateua kamati itakayosimamia mambo ya katiba, sheria nanidhamu ya umoja.
6.4 Kamati ya utendaji itakuwa na wajibu wa kuunda kamati mbalimbali zitakazo imarisha
utendaji wa umoja.
6.5 Kiongozi anaweza kuongoza mihula miwili kama ataonekena anafaa kufanya hivyo na
wanaumoja.

WAJIBU WA VIONGOZI.

MWENYEKITI.
a.       Mwenyekiti; ataendesha vikao vyote vya umoja ndie msemaji mkuu katika mikutano yote na kutoa miongozo kwa kila jambo ndani na nje ya mkutano wa umoja.
b.      Mwenyekiti; msaidizi huyu atafanya shughuli zote za mwenyekiti kwa kutumwa na mwenyekiti au pindi mwenyekiti anapokuwa hayupo.



KATIBU.
a.       Katibu, atakuwa ndiemtendaji mkuu wa umoja kwa shughuli zote zakiutendajikwa wana umoja pia ataandika taarifa zote za mikutano na kutunza kumbukumbu zote za vikao halali vya umoja,na atakuwa na mawasiliano ya marakwamara kati ya uongozi na  wanaumoja kuhusu taarifa zozote zinazo wahusu wanaumoja.

b.      Katibu msaidizi atafanya shughuli zote za katibukwa kushirikiana na pindi katibu mkuu atakapokuwa hayup atakaimu.

MTUNZA HAZINA.
a.       Atahakikisha anafuata taratibu zote za uhifadhiwa fedha za umoja.
b.      Atapokea pesa na kutoa risiti kwa mwanaumoja yeyote atakae toa pesa zihusuzo umoja.
c.       Atafanya malipo pale atakapo takiwa kufanya hivyo na kamati ya fedha ya umoja kwa kushirikiana na watia saini baada ya kulipishwa na kamati ya utendaji.
d.      Atahakikisha hesabu zote za fedha ya umoja ndiye atazitolea maelezo ya mapato na matumizi pale atakapotakiwa kufanya hivyo na kikao halali cha umoja.
e.       Atatunza vitabu vyote vya risiti na hesabu za umoja.
f.       Atakusanya na kupeleka pesa bank  kila mara.
g.      Ataandaa hesabu zote za umoja na kuziwakilisha kwenye kikao/mkutano husika.
h.      Atashauri kamati ya fedha juu ya matumizi ya umoja yenye tija.
i.        Atashirikiana na kamati ya fedha kuandaa bajeti ya matumizi ya umoja pale inapotakiwa kufanya hivyo.
j.        Atafanya kazi kwa kufuata taratibu za umoja chini ya mwenyekiti na katibu wa Uwawase Group.



KAMATI YA UTENDAJI.
Kamati hii ndiyo kamati ambayo inatakiwa kuwa makini kwa kuhakikisha inafanya mambo ya kiutendajizaidi.
1.      Itapokea na kutekeleza maelekezo yote kutoka mkutano mkuu wa umoja
2.      Itafuatilia kazi na maelekezo mbalimbali yanayo husu umoja wetu
3.      Itahusika kutoa maelekezo ya kiutendaji kwa kamati mbalimbali za umoja wetu.
4.      Itaitisha mkutano wa dharura kujadili jambo lolote jipya kwa wanaumoja.
5.      Itakuwa na jukumu la kumuhidhinisha mwanaumoja mpya baada ya kupokea barua yake ya maombi ya kujiunga na umoja iliyokuwisha  jadiliwa na kamati ya katiba  na sheria.
6.      Itabuni na kuanzisha mradi au jambo lolote maslahi kwa wanaumoja baada ya kukubaliwa na mkutano mkuu.
7.      Itazingatia maslai ya umoja zaidi kuliko vinginevyo.


KAMATI YA KATIBA SHERIA NA NIDHAMU.
Kamati hii itakuwa ndiyo msingi wa umoja wetu kwa kuhakikisha inafanya mambo yake kwa werevu  mkubwa huku ikijuwa kuwa ndio tegemeo kubwa la kisheria la umoja, nayo itateuliwa kupitia mkutano mkuu wa wanaumoja, hatahivyo itakuwa kamati huru, kamati hii itasimamia uchaguzi wa viongozi  kipindi cha uchaguzi, pia itafanya yafuatayo:-
a.       Kusimamia utekelezwaji wa maelekezo ya katiba ya umoja.
b.      Kusimamia maboresho ya katiba ya umoja pindi itakapo lazimika kufanya hivyo.
c.       Kuhakikisha kila kiongozi/mwanaumoja anatii na kufuata sheria hizo
d.      Kudhibiti mwiingiliano wa uongozi katika umoja.
e.       Kuunda sheria ndogondogo zitakazo ongoza umoja wetu.
f.       Kuhakikisha viongozi wa umoja wanatii na kuilinda katiba katika utendaji wao
g.      Kusimamia adhabu kwa mwana umoja kutokana na kosa alilofanya.
h.      Kushauriana na kamati ya utendaji juu ya kufanya mikataba mbalimbali inayohusu umoja wetu.
i.        Kupokea na kujadili barua ya barua ya maombi mapya kabla ya kuidhinishwa na kamati ya utendaji.

j.        Kamati hii pamoja na kuwa huru itafanya kazi kwa karibu na chini ya kamati ya utendaji kwa maslahi ya wanauwawase group.


Share:

UENDESHAJI WA MASUALA YA KIFEDHA NDANI YA UWAWASE GROUP


UENDESHAJI WA MASUALA YA KIFEDHA NDANI YA UWAWASE GROUP





    VYANZO VYA MAPATO.
1.      Kiingilio.
2.      Ada.
3.      Mikopo ya bank/Taasisi za fedha.
4.      Msaada toka kwa wafadhili
5.      Mauzo ya nakala ya katiba.
6.      Mauzo ya vitabu vya sheria ndogondogo za umoja.
7.      Michango mbalimbali kutoka kwa taasisi zisizokuwa za serikali za ndani na nje ya nchi, vitu halisi au fedha.

4.1 MATUMIZI YA MAPATO.
Umoja huu uta hakikisha una yatumia ipasavyo mapato yote yaliyopatikana kwa njia tajwa hapo juu yaani (4.0 1hadi 7)kwa kufanya mambo yafuatayo:-
1.      Kulipa pango la ofisi ya Uwawase Group.
2.      Kumpa rambirambi mfiwa au marehemu kwataratibu tuliojiwekea.
3.      Kusaidia jitihada za kutafuta malighafi (mahindi) popote pale ili kuwafanya wanaumoja kupata mahindi hasa kipindi cha upungufu wa mahindi.
4.      Ikibidi hata kufanya mawasiliano na nje ya nchi kufanikisha kupata mahindi.
5.      Kuendesha shughuli zote za ofisi ya UWAWASE GROUP, pamoja na kugharamia matumizi ya ofisi.
6.      Kulipa watumishi wa ofisi kama Karani/Secretary, mlinzi, na viongozi kwa shughuli maalum za ofisi na ufuatiliaji nje ya ofisi kwa manuafaa ya umoja wetu.
7.      Ikifikia wakati tuibue vitega uchumi mbalimbali kuimarisha mfuko wetu.
8.      Kugharamia mikutano yote ya Uwawase Group.
9.      Kutimiza malengo ya umoja yaliyopitishwa na mkutano mkuu.



4.2 VITU HALISIYA.
a)      Iwapo mtu au taasisi itafanya shughuli na UWAWASE GROUP na ikafanikiwa kujitolea vifaa au pesa, kwaajili ya utekelezaji wa mpango wowote UWAWASE GROUP haitalipa wala kugharamia uharibifu wowote utakaojitokeza.

b)      UWAWASE GROUP itabaki kuwa ndio mmiliki mkuu wa mali na wanaumoja wake,bila kuingiliana na taasisi yoyote ile iliyoshirikishwa.

4.3 ASASI ZA FEDHA.
a)      Iwapo mkutano mkuu ukiona kuna umuhimu wa kupatapesa kutoka benki kwa haraka katika umoja wetu kwaajili ya kufanya jambo kwa maramoja na lenye malengo mema kimaendeleo, basi mkutano mkuu utatoa idhini kwa kamati ya utendaji kufanya hivyo chini ya taratibu ambazo mkutano mkuu utakuwa umeziweka/kuridhia kwa pamoja.

b)      Wanaumoja watakaopitisha azimio hili la kukopa pesa au bank katika Taasisi kipesa zilizoruhusiwa kisheria lazima liwe theluthi tatu ya wanaumoja wote.



4.4 UHIFADHI WA FEDHA.
1.      Umoja utahifadhi pesa zake bank.
2.      Sehemu ya pesa ndogondogo zinazohitajika kwa matumizi ya kiofisi yatahifadhiwa kwa taratibu zitakazowekwa na uongozi kwa mtunza fedha,
3.      Tunaweza kuwekeza fedha kwa kununuwa hisa au mali isiyo hamishika kama nyumba, kiwanja/shamba kwa makubaliano ya wanaumoja kupitia mkutano mkuu.
4.      Mwaka wa fedha wa umoja utaanza Januari na kuishia DIsemba.
5.      Umoja utaandaa hesabu zake na kuzitunza kwa utaratibu ulioandaliwa na wanaumoja wenyewe.
6.      Kamati ya mipango, uchumi nafedha ya umoja itapitia taarifa ya fedha kila baada ya miezi mitatu na kuiwasilisha kwenye mkutano wa wanaumoja.
7.      Wajumbe wa kamati yamipango, uchumi na fedha watakuwa na idhini ya kupitia manunuzi, matumizi, na mapato yote yaliyofanyika kwenye umoja.
8.      Ukaguzi,kuundwe kamati ya dharura ya ukaguzi wa hesabu za mwaka kutoka kwa wana umoja wenyewekamati hiyo isizidi watu watano kwa ukaguzi wa hesabu za ndani(mtaalam wa hesabu/mahesabu).
9.      Muda wa kamati ya ukaguzi utakoma baada ya kumaliza hesabu hizo ndani ya mwezi mmoja.

10.  Gharama za kamati ya ukaguzi zitalipwa na mfuko wa umoja wenyewe.
Share: