Thursday, April 28, 2016

MADHUMUNI YA KUANZISHA UWAWASE GROUP

MADHUMUNI YA KUANZISHA UWAWASE GROUP




1 Madhumuni ya umoja huu ni kuhakikisha  kuwa wazalishaji wa Sembe/Dona na wamiliki wa mashine za kuzalishaSembe tunakuwa na chombo cha kutusemea kwa umoja wetu na kutufanya tuwe pamoja na kutuwezesha kusaidiana pale inapo tokea kunahaja ya kusaidiana, kwa ugonjwa au kifo. Pia ni kuhakikisha tunaendesha umoja wetu huu kwa kufuata misingi na sheria za nchi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, mbali na yote umoja wetu utalazimika kufanya mambo yafuatayo;-
a.       Kununua mahindi popote yatakapo patikana ndani na nje ya nchi.
b.      Kuuza sembe na dona ndani na nje ya inchi kwa kufuata sheria za nchi.
c.       Kutii mamlaka za serikali na kufuata maagizo yake.pamoja na kupokea maelekezo toka manispaa kwa utekelezaji.
d.      Kutetea na kulinda maslai ya wana uwawase
e.       Kukusanya ada na michango mingine itakayoidhinishwa na mkutano mkuu  kwa wana umoja wote. Ili kuboresha utendaji wa umoja wetu.
f.       Kutekeleza maamuzi ya takayo pitishwa kwenye mkutano mkuu wa wanaumoja .


Share:

0 comments:

Post a Comment